Alhamisi 12 Machi 2026 - 12:30
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kwa Mtukufu Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei

Hawza/ Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon katika ujumbe wake kwa Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei alimpongeza kwa kuchaguliwa kwake kuwa Kiongozi wa tatu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naeem Qassim, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, katika ujumbe wake alimpongeza Mtukufu Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei kwa kuchaguliwa na Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis-e Khobregan) kuwa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika ujumbe huo alisisitiza kwamba uchaguzi huu unaendeleza njia ya Imam Khomeini na Imam Sayyid Ali Khamenei; njia ambayo imefuatwa kwa ajili ya kulinda uhuru wa Iran, utambulisho wa Kiislamu na kupambana na dhulma pamoja na uvamizi.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, huku akirejelea namna Hizbullah ilivyopata msukumo kutoka katika Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alitangaza kwamba, harakati hiyo itaendelea kubaki mwaminifu kwa uongozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu kama ilivyokuwa hapo awali, na akasisitiza kuendelezwa kwa uungaji mkono kwa mhimili wa muqawama pamoja na kupambana na dhulma na ukaliaji wa mabavu.

Sheikh Naeem Qassim pia kwa niaba ya Baraza la Hizbullah, uongozi wake na vikosi vya muqawama wa Kiislamu nchini Lebanon, alifanya upya bay’ah (kiapo cha utii) kwa Kiongozi mpya wa Iran, na akamtakia mafanikio katika kutekeleza malengo na matarajio ya watu wa Iran pamoja na wanyonge wote duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha